Takriban watu sita wamefariki wanne kati yao wakiwa ni Walimu wa Shule ya Msingi Lumalu iliyopo Kata ya Upolo Wilaya Nyasa Mkoani Ruvuma, baada ya kutokea ajali ya gari katika Kijiji Cha Chunya Wilayani Mbinga.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, Peres Magiri amesema gari aina ya Prado yenye namba za usajili T 647 CVR iliwaka moto majira ya saa 2 asubuhi hii leo Desemba 28, 2024 katika Kijiji hicho.

Amesema, Walimu hao walikuwa wakielekea Makao Makuu ya Wilaya ya Nyasa Kilosa na kuwataka kwa majina kuwa ni Vicent Alel Milinda aliyekuwa Dereva na Boniface Bosco Mapunda.

Wengine ni Walimu hao wanne ambao ni Damas Nambombe, Dominica Abeat Ndau, Judith Joseph Nyoni, na John Sylvester Mtuhi na Juhudi za kumtafuta Kamanda wa Polisi Mkoani Ruvuma zinaendelea ili kujua undani wa tukio hilo.

Tetesi za Usajili Dunia Disemba 30
Aliyeuwa 27 aachiliwa huru, Raia wasema wanajua la kufanya