Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Ammy Nyamisenda ametoa wito kwa Vijaya kutambua nafasi yao kama nguvu kazi muhimu kwa maendeleo ya taifa na familia zao likiwemo suala la ulinzi wa maeneo yao.
Nyamisenda ametoa wito huo wakati akizungumza na vijana wa kata ya Itaba Wilayani Kibondo Mkoa wa Kigoma.
Amewaambia Vijana hqo kuwa wanapaswa kuchukua jukumu la kujiingiza katika shughuli za uzalishaji ili kujipatia kipato.
“Kukaa kijiweni hakutawasaidia kufanikisha malengo yao bali ni kupoteza muda kwa kushabikia stori za uongo ambazo haziwasaidii Katika maendeleo yenu,” alisema Mkaguzi Msaidizi Nyamisenda.