Chuo Kikuu Mzumbe kimewatoa hofu wanafunzi ambao hawajafanya usajili chuoni hapo kwamba zoezi la usajili bado linaendelea mpaka January 10, 2025 na wapuuze taarifa zinazosambaa mtandaoni.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Willium Mwegoha, akizungumza na waandishi wa habari amekanusha taarifa zilizopo kwenye mitandao ya kijamii kwamba wanafunzi wanaotakiwa kuendelea na usajili ni wale tu wanapata mkopo kutoka serikalini.
Amesema kuwa taarifa hizo zimesababisha mkanganyiko mkubwa kwa baadhi ya wanafunzi na kwamba barua hiyo inayosambaa mtandaoni ipuuzwe. “Taarifa hizi hazina ukweli wowote. Menejimenti ya chuo iliamua kuongeza muda wa usajili kwa wanafunzi wote bila ubaguzi,” alisema Prof. Mwegoha.
Ametoa ufafanuzi huo baada ya kuzuka kwa taarifa potofu kwenye mitandao ya kijamii, zikidai kuwa muda wa kujisajili umeongezwa hadi Januari 10, 2025, kwa Wanafunzi wenye sifa za kupata mikopo ya serikali pekee.
Aidha, Prof. Mwegoha amesema tayari wanafunzi 900 kati ya 1,636 wamejisajili tangu muda wa usajili ulipoongezwa huku akitoa wito kwa wanafunzi waliobaki kuhakikisha wanakamilisha mchakato wa usajili kabla ya muda kufikia kikomo.
Chuo Kikuu Mzumbe kimeendelea kusisitiza kuwa ni muhimu kwa wanafunzi kufuata taarifa rasmi kutoka kwa uongozi wa chuo ili kuepuka taharuki zinazotokana na uvumi usio sahihi.

Wala kiapo kutofumbia macho uhalifu
Habari kuu katika Magazeti ya leo Janauri 10, 2025