Zikiwa zimebaki siku chache shule zifunguliwe, Jeshi la Polisi mkoa wa Manyara limetoa wito kwa wamiliki wa wa Shule kuhakikisha magari ya kubeba wanafunzi yanakaguliwa, ili kudhibiti ajali za barabarani.

Kamanda wa usalama barabarani Mkoa Manyara, Michael Mwakasungula amesema jeshi hilo limejipanga kufanya ukaguzi wa kutosha kwa magari ya Shule na vyombo vingine vya moto, ili kudhibiti ajali ambazo zinaweza kutokea kutokana na uzembe.

Aidha, Mwakasungula amewataka wazazi wanaotumia usafiri wa bodaboda kusafirisha Wanafunzi kuacha mara moja kwani usafiri huo si salama Kwa wanafunzi ambapo amesema hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Aidha, katika hatua nyingine pia amewataka madereva wa vyombo vya moto mkoanihumo kufuata Sheria zote za usalama barabarani.

Umeme Nyumba kwa Nyumba: REA yaendelea kuhamasisha Wananchi
Maisha: Mimba tata nyumbani kwa Bosi wangu