Sina shaka umewahi kutazama juu na kuona pete kubwa ya mwanga unaozunguka jua au mwezi na kama ulikuwa makini basi hata Jumapili ya Januari 12, 2025 tukio hili limeonekana kwa badhi ya maeneo ikiwemo jijini Dar es Salaam.

Wanasayansi hutaja tukio hili kama halos za digrii 22 na walipata jina hilo kwa sababu eneo ya duara lililo na takriban digrii 22 ya mtazamo huu usio wa kawaida unasaobabishwa na mawingu haya yaliyo umbali wa futi 20,000 (kilomita 6) au zaidi angani.

Kuna tafsiri ya zamani ya Watu wa hali ya hewa wakisema uwepo wa pete karibu na mwezi hunamaanisha ujio wa mvua katika siku za usoni na kuna ukweli kwenye utabiri huu, kwa sababu mawingu ya juu ya cirrus mara nyingi huja kabla ya mvua.

Mawingu haya yana mamilioni ya fuwele ndogo za barafu na Halos unazoziona husababishwa na mwonekano wa nyuma, au mgawanyiko wa mwanga na pia kwa kuakisi au kumeta kwa mwanga kutoka kwa fuwele hizi za barafu. Fuwele lazima zielekezwe na kuwekwa sawa, ili halo ionekane.

Tahadhari.

Kwa wenye kamera jihadharini wakati wa kupiga picha za tukio hili kwani kuelekeza kamera moja kwa moja kwenye jua lisilofichwa kunaweza kuiharibu na kamwe usiangalie jua moja kwa moja, hata wakati lina mwanga kidogo kupitia mawingu au ukungu.

Halos inaweza kutokea popote kwenye sayari wakati wa baridi au kiangazi na ikiwa ina fuwele zinazounda halo ingawa ni ngumu pia kutabiri kwa mfano, kuna tofauti kubwa katika masafa ya halo na aina za halo katika umbali wa kilomita 300 ukiwa upo Nchini U.K.

Utambuzi.

Kwa sababu mwanga wa mwezi sio mkali sana, halo za mwezi mara nyingi hazina rangi. Hata hivyo, unaweza kuona rangi nyekundu ndani na bluu nje ya halo na rangi hizi hunaonekana zaidi katika halos karibu na jua.

Ikiwa unaona halo karibu na mwezi au jua, angalia kwamba makali ya ndani ni mkali, wakati makali ya nje yanaenea zaidi na ni mepezi yaani hayaumizi macho lakini pia, ona kwamba anga inayozunguka halo ni nyeusi kuliko anga nyingine.

Mapokezi Wakuu wa Nchi 53 za Afrika: Tanzania ipo tayari
Maisha: Kisa 2000 Mwanaume apagawa