Viongozi mbalimbali wa dunia wapongeza makubaliano ya kusitisha mapigano kwa wiki sita huko Gaza na kuachiliwa kwa mateka, ambayo yataanza kutekelezwa rasmi Jumapili ya Januari 19, 2025.
Makubaliano hayo ya kihistoria, yanajumuisha hatua tatu za kufanikisha kuvimaliza kabisa vita hivyo ambapo katika hatua ya kwanza ni kuwachiliwa kwa mateka 33 wa Israel, ambao wanashikiliwa na Hamas pamoja na wafungwa wa Kipalestina.
Kufuatia mafanikio hayo, Viongozi wa Mataifa mbalimbali Duniani wamepongeza wakisema yanatoa matumaini kwa raia wa pande zote walipitia mateso na kwamba yatasaidia kuendeleza juhudi za kufanikisha amani ya kudumu, kati ya Israel na Palestina.
Hata hivyo, wakati hayo yakijiri inaarifiwa kuwa watu 12 wameuawa hii leo Januari 16, 2025 huko kaskazini mwa Ukanda wa Gaza, baada ya Israel kushambulia kwa makombora jengo la makazi na kuzua sintofahamu.