Wazazi na walezi Nchini, wamekumbushwa kutoa malezi bora kwa vijana wao ili kukuza jamii yenye upendo na kuchukia vitendo vya kiuhalifu.
Hayo yamebainishwa na Mkaguzi Kata ya Kisangura Wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Genuine Kimario katika Kata ya ya Kisangura iliyopo Wilayani Serengeti Mkoani Mara.
Amesema, wazazi na walezi wanatakiwa kuendelea kutoa malezi bora ikiwa ni pamoja na kuwapa elimu watoto wao na kuendelea kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili kata hiyo iendele kuwa salama.
Kimario ameitoa elimu hiyo katika kampeni yake ya nyumba kwa nyumba, ikilenga kuwakumbusha wazazi na walezi katika kuwalea watoto katika misingi bora na kuwapa elimu ambayo itawakomboa kifkra.

Changamoto: Wanahabari 67 wanafungwa jela
Makosa udhalilishaji wa Kijinsia yamepungua – DCI Chembera