Makosa dhidi ya binadamu yamepungua ambapo katika kipindi cha Januari hadi Disemba, 2024 yameripotiwa jumla ya makosa 1,116 katika Vituo vya Polisi Zanzibar, ikilinganishwa na makosa 1,280 ya kipindi kama hicho mwaka 2023 sawa na upungufu wa makosa 164ambayo ni asilimia 12.8 yakiwemo ya kubaka na kulawiti.
Akitoa tathimini ya hali ya usalama Zanzibar kwa kipindi cha Januari hadi Disemba 2024 huko Makao Makuu ya Polisi Zanzibar, Naibu Kurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Naibu Kamishna wa Polisi, Zuberi Chembera amesema katika kipindi cha Januari hadi Desemba 2024 Jumla ya makosa 829 ya kubaka yameripotiwa ikilinganishwa na makosa 927 ya kipindi kama hicho mwaka 2023 ni upungufu wa makosa 98 sawa na asilimia 10.6.
Amesema, katika kipindi cha Januari hadi Desemba 2024 Jumla ya makosa 217 ya kulawiti yameripotiwa ikilinganishwa na makosa 309 ya kipindi kama hicho mwaka 2023 ni upungufu wa makosa 92 sawa na asilimia 29.8.
Hata hivyo, DCP Chembera amesema makosa dhidi ya binadamu kwa upande wa makosa ya mauaji yameongezeka ambapo katika kipindi cha Januari hadi Disemba 2024 Jumla ya makosa 66 yameripotiwa ikilinganishwa na makosa 44 ya mwaka 2023 ikiwa ni ongezeko la makosa 22 sawa na asilimia 50 ambayo mengi yametokana na baadhi ya wananchi kujichukulia sheria mikononi.
Aidha, amewataka Makamanda wa Polisi wa Mikoa pamoja na Maafisa wa Polisi kuongeza nguvu katika kuzuia makosa ya Mauaji, wizi wa pikipiki, wizi wa mifugo, makosa dhidi ya watalii na makosa ya usalama barabarani ambayo yameongezeka mwaka 2024 ikilinganishwa na mwaka 2023.

Wakumbusha kutoa elimu, malezi bora kwa Watoto
Sita wahukumiwa kunyongwa kwa mauaji