Ushindi wa mabao 2-0 walioupata Simba dhidi ya Cs Constantine umeifanya klabu hiyo kufikisha alama 13 na kuongoza kundi A la kombe la Shirikisho barani Afrika. Mabao ya Kibu Denis dakika ya na Lionel Ateba dakika ya yaliifanya Simba iendelee kuutumia vyema uwanja wa Benjamin Mkapa kwa kuondoka na alama 9 katika michezo mitatu ya makundi.
Msimu wa 2024/25 Simba chini ya kocha Fadlu Davis imefanikiwa kushinda michezo 4 sare 1 na kupoteza 1 wakifunga jumla ya mabao 8 na kuruhusu mabao 4 pekee.Mshambuliaji Kibu Denis ndiye kinara wa mabao kwa Simba akifunga mabao 3 akifuatiwa na Lionel Ateba mabao 2 sawa na Jean Charles Ahoua na Mohammed Hussein akifunga bao moja.
Simba alipaswa kushinda mchezo huo muhimu ili aweze kumaliza nafasi ya 1 na kuwakwepa vigogo kama Zamalek aliyeongoza kundi D, USM Alger aliyeongoza kundi C kwa alama 14 na RS Berkane aliyemaliza kundi B akiwa na alama 16. Kama Simba angeshika nafasi ya pili basi angekuwa na wakati mgumu na ushindi mkali kutoka kwa vigogo hawa wa soka.
Tunaiona Simba ikifika nusu fainali na fainali
Klabu ya Simba ina nafasi kubwa ya kuingia nusu fainali msimu huu.Yawezekana hii ndiyo robo fainali nyepesi zaidi kwa Simba kwa kipindi cha hivi karibuni. Katika hatua hizi Simba inaweza kupangwa na Asec Mimosa,Al Masry au Stellenbosch.Nimewatazama wapinzani hawa wa Simba na ninaona ni wepesi mno kulinganisha na Simba hii.
1.Simba ikipangwa na Stellenbosch
Stellenbosch ni timu kutoka Afrika ya kusini na msimu huu walipangwa kundi B wakishinda michezo 3 na kufungwa 3,Klabu hiyo ilifungwa jumla ya mabao 10 na kufunga mabao 6 pekee ikikusanya alama 9.Kundi B liliundwa na kigogo mkongwe mmoja ambaye ni RS Berkane aliyevuna alama 16. Stellen alishinda didi ya Lunda Sul na Stade Malien . Stellenbosch ni timu ya kawaida sana na Simba watakuwa na nafasi kubwa ya kushinda michezo ya nyumbani na ugenini. Simba haijawahi kucheza na Stellenbosch lakini uzoefu wa kocha Fadlu kwa soka la Africa Kusini italeta chachu katika mchezo huo
2.Simba ikipangwa na ASEC Mimosa
Simba na Asec Mimosa wamekuwa wakikutana mara kwa mara kwa siku za hivi karibuni. Timu hizo zimekutana katika makombe ya Shirikisho na Ligi ya mabingwa . Timu hizo zimecheza jumla ya mechi 4 kila mmoja akishinda mchezo mmoja wakitoka sare mara mbili. Michezo ya mwisho kukutana ni msimu wa 2023/24 hatua ya makundi ligi ya mabingwa Afrika na katika michezo yote miwili walitoka sare.
Msimu huu Asec Mimosa amemaliza nafasi ya 2 kundi C nyuma ya USM Alger. Asec walishinda mechi mbili pekeee za kundi sare 2 na kufungwa 2 wakifunga mabao 7 na kuruhusu mabao 5.Asec Mimosa ya msimu huu si hatari sana kwa Simba.
3.Simba ikipangwa na Al Masry
Al Masry ya Algeria si ngeni kwa Simba ,Timu hizo zilikutana hatua ya makundi kombe la Shirikisho msimu wa 2017/18.Mchezo wa kwanza uliopigwa dimba la Benjamin Mkapa ulimalizika kwa sare ya 2-2 na mchezo wa pili ulimalizika 0-0. Simba wana nafasi kubwa sana ya kufanya makubwa kwenye mchezo huo kutokana na udhaifu wa Al Masry waliouonyesha hatua ya makundi kwa kushinda mechi 2 sare 3 na kufungwa mchezo mmoja wakifunga mabao 7 na kuruhusu mabao 4.
Kama Simba wataendelea kuwa na kiwango bora kama walichoonyesha kwenye mchezo dhidi ya CsConstantine basi hatua ya robo fainali 9itakuwa nyepesi sana . Niliwatazama Ellie Mpanzu na Kibu Denis namna wanavyotumika kupandisha mashambulizi kutokea pembeni na uwezo wao wa kusogea mpaka eneo la kati na kucheza kama washambuliaji wa mwisho namna wanavyotumia akili ,nguvu na ufundi mwingi naiona safu ya ushambuliaji ikizidi kuwa bora zaidi.
Yusuf Kagoma na Fabrice Ngoma wameendelea kuiva vyema kwenye chungu cha Fadlu,wanaifanya safu ya kiungo ya Simba kuzidi kuimarika zaidi na wamecheza kwa weledi nyakati zote.tutegemee makubwa zaidi kutoka kwao.