Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema katika muongo mmoja uliopita, Tanzania imepiga hatua katika kuboresha huduma za afya kwa jamii katika sekta ya afya.
Rais Dkt. Samia ameyasema hayo wakati yeye na mgeni wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika laAfya Duniani (WHO), Dkt. Tedros Ghebreyesus wakizungumza na vyombo vya Habari, IkuluChamwino Mkoani Dodoma.
Amesema, juhudi za Serikali katika kupunguza vifo vya wajawazitozimesaidia kutoka vifo 556 hadi vifo 104 kwa kila vizazi hai 100,000.
Rais Dkt. Samia pia amesema jitihada hizo zimechangiwa na Serikali kuwekezakatika miundombinu ya afya ambapo imewezesha asilimia sabini ya wananachi kuwezakupata huduma za afya ya msingi ndani ya umbali wa kilomita tano.
Rais Dkt. Samia pia amesema vifo vya Watoto chini ya umri wa miaka mitano vimepungua.kutola asilimia sitini na saba hadi asilimia arobaini na tatu kati ya vizazi hai 1,000.
Hata hivyo, vifo vya watoto wanaozaliwa kabla ya wakati vimepungua kwa kasi ndogo huku Rais Dkt. Samia akisema Tanzania inafungamana na mapendekezo ya WHO kuanzisha vitengo vya kuhudumia watoto wachanga hususan wanaozaliwa kabla ya mudahadi kufikia asilimia themanini ya vituo vinavyotoa huduma za Afya.
Mwaka 2024 Tanzania ilipiga hatua muhimu katika kuhakikisha huduma za afya zinapatikanakwa watu wote kwa kuzindua mpango jumuishi na shirikishi wa wahudumu wa Afya ngazi yaJamii utakaowafikishia wananchi huduma za Kinga, Tiba na Elimu ya Afya mahali walipo bilavi kwazo.