Wawakilishi wa mshambuliaji wa Uingereza Marcus Rashford walikutana na viongozi wa Barcelona siku ya Jumanne huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 akitafuta njia ya kuondoka Manchester United. (Sky Sports)

Arsenal inamfuatilia kwa karibu mshambuliaji wa Slovenia na klabu ya RB Leipzig ya Ujerumani Benjamin Sesko, 21. (Sportsport)

AC Milan imefikia mkataba wa kumsajili beki wa Uingereza Kyle Walker, 34, kutoka Manchester City ambao utakuwa mkopo wa awali lakini unajumuisha chaguo la kununua kwa euro 5m (£4.2m). (Sky Sports Italia)

 Kyle Walker

Winga wa Manchester United Alejandro Garnacho anapendelea kuhamia Chelsea badala ya Napoli, ambako ombi lao la kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina mwenye umri wa miaka 20 limekataliwa. (TyC Sports, kupitia Metro)

Napoli pia inpania kumsajili winga wa Ujerumani Karim Adeyemi, 23, kutoka Borussia Dortmund. (Fabrizio Romano)

Wachezaji watatu wa Chelsea huenda wakakihama klabu hicho mwezi huu huku mlinzi wa Ureno Renato Veiga, 21, akishinikiza kuungana na Juventus (Mail)

Nottingham Forest inaandaa dau la kubbwa ambalo huenda likafikia pauni milioni 60, ili kumsajili mshambuliaji wa Brazil Matheus Cunha, 25, kutoka Wolves. (Sky Sports)

Juventus wameipa Chelsea fursa ya kumsajili kiungo wa kati wa Brazil Douglas Luiz, 26, ambaye pia ananyatiwa na Manchester City na Arsenal. (TeamTalk)

Kiungo wa Ufaransa Paul Pogba, 31, anazingatia ofa kadhaa kutoka kwa timu za ligi tano kuu za Ulaya, lakini makubaliano ya mkataba hayajafikiwa. (ESPN)

Mustakabali wa mkurugenzi wa ufundi wa West Ham Tim Steidten katika klabu hiyo uko mashakani baada ya The Hammers kukamilisha dili la kumsajili mchambuzi wa masuala ya uajiri wa Chelsea Kyle Macaulay, ambaye amewahi kufanya kazi na kocha Graham Potter. (Guardian)

Juventus wameipa Chelsea fursa ya kumsajili Douglas Luiz

Chanzo cha picha,Getty Images

Maelezo ya picha,Juventus wameipa Chelsea fursa ya kumsajili Douglas Luiz

Everton wameonyesha nia ya kumsajili winga wa Sporting Muingereza Marcus Edwards, 26. (), kutoka Caught offside)

Wakala wa Emerson Royal wa AC Milan, 26, amezungumza na Everton na Fulham, lakini beki huyo wa Brazil pia analengwa na Galatasaray. (Calciomercato – kwa Kiitaliano)

Manchester United wanatathmini iwapo watawasilisha dau lililoboreshwa la kumnunua beki wa Lecce Patrick Dorgu baada ya ombi la awali la mchezaji huyo wa kimataifa wa Denmark kukataliwa. (Star)

Lakini Napoli wanatumai kuipiku Manchester United kupata saini ya Dorgu. (Gazzetta dello Sport – kwa Kiitaliano)

Inter Milan::Rekodi ya mkongwe wa Brazil yafikiwa na nyota wa Argentina
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Januari 23, 2025