Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Julius Mtatiro amewataka wazazi na walezi kuhakikisha wanawapeleka watoto wenye sifa ya kujiunga na shule ya awali na msingi, ili waweze kupata haki yao ya kupata elimu.

Mtatiro ameyasema hayo wakati akiwa katika ziara yake ya kikazi ya kusikiliza na kutatua kero za wannachi kwenye Kijiji cha Ibanza Kata ya Mwamala ambapo amesisitiza wazazi na walezi kuhakikisha wanatekelea hilo bila kujali visingizo vya kutokuwa na sare za shule na kwamba tayari imeanzishwa oparesheni maalumu kwa watakaokiuka agizo hilo.

Amewataka wazazi na walezi kushirikiana na Kamati Maalumu ya lishe ili kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula shuleni kwa lengo la kuwategenezea mazingira Rafiki na wezeshi ya kusoma vizuri.

Amesema, “tumeshaidhinisha oparesheni tayari, na oparesheni hii ukiichezea itakutia kweye misukosuko kwa sababu hujapeleka mtoto shuleni, peleka mtoto shuleni hata kama hana shati la shule atapokelewa shuleni utaandika barua lini utampatia mtoto shati la shule,

pia kuna zile kamati za wazazi ambazo zinahakikisha Watoto wanapata lishe shuleni usisubiri kugombana na Mkuu wa Shule hakikisha mnatoa ushirikiano wa kutosha kuhakikisha Watoto wanapata lishe shuleni na hili pia ni agizo la serikali mtoto mwenye njaa hawezi kufundishika”.

Aidha katika hatua nyingine, DC Mtatiro ameagiza wazazi na walezi hao kuhakikisha Watoto wote wa kike wenye umri wa kuanzia miaka 9 hadi 14 wanawapeleka Hospitali kupata chanjo ya Saratani ya Shingo ya Kizazi, ili kuwakinga na athari za ugonjwa huo na kuachana na tabia ya kuwakataza Watoto wao kupata chanjo hiyo.

NECTA yatangaza matokeo ya Kidato cha nne
UEFA: Kikosi cha Guardiola kina hali mbaya baada ya kusambaratishwa na PSG