Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), Dkt. Said Mohamed amesema idadi ya watahiniwa waliopata daraja la IV na zero imepungua, hivyo ubora wa ufaulu umepanda kwa asilimia 5.6.

Dkt. Mohamed ameyasema hayo hii leo Januari 23, 2025 na kudai kuwa ubora wa ufaulu wa jinsi, kwa kuzingatia ufaulu wa madaraja ya I-III, wavulana ni 119,869 sawa na asilimia 54 na wasichana ni 102,084 sawa na asilimia 46.

Amesema, Wasichana wamefaulu wengi huku Wavulana wakifaulu vizuri zaidi, ambapo kwa mwaka 2024, takwimu zinaonesha idadi ya watahiniwa waliopata madaraja ya I, II na III imeongezeka na kufikia 221,953 sawa na asilimia 43, ikilinganishwa na mwaka 2023 ambapo idadi ilikuwa 197,426 sawa na asilimia 37.4.

Aidha, Dkt. Mohamed amefafanua kwamba kati ya watahiniwa 477,262 waliofaulu mtihani wa Kidato cha Nne, wasichana ni 249,078 sawa na asilimia 52, na wavulana ni 228,184 sawa na asilimia 48.

Kuhusu ufaulu, Dkt. Mohamed amessma umepanda kwa asilimia 3 hadi kufikia asilimia 92.3 kwa jumla, ambapo watahiniwa 477, 262 wamefaulu kidato cha nne kati ya wahitimu 516, 695.

Huduma za fedha Vijijini: Serikali yatoa darasa Endabash
Ramovic apigilia msimamo wake kuhusu Ligi kuu ya NBC