Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega leo Januari 23, 2025 amezindua mashirikiano kati ya Serikali na Sekta binafsi katika kituo cha Magogoni kwa kuzindua rasmi vivuko viwili ambavyo vitatoa huduma kwa Wananchi, uwekezaji ambao umefanywa na Azam Marine.

Akiongea wakati wa hafla hiyo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema wameona namna watanzania wanavyohangaika kwa kuwa bado Serikali ilikuwa haijatoa majawabu sahihi ya changamoto za vivuko.

Amesema rasmi leo imejidhihirisha kupitia uzindua vivuko hivyo 2 Sea Tax 3 na Sea Tax 4 pamoja na kuweka mfumo wa kidijitali wa kukatisha Risiti na Kituo cha Kisasa cha Abilia kusubiria vivuko.

“Huo ni uwekezaji unaojibu changamoto za wananchi naipongeza sana Azam Group niwaombe muendelee kuwekeza na maeneo mengine,” alisema RC Chalamila.

Aidha RC Chalamila amesema TANROAD wana maeneo ya hifadhi za barabara ambayo ni vichaka, hivyo ameshauri maeneo hayo wapewe watu ambao wako serious na uwekezaji ambao utakuwa na tija na masilahi mapana kwa umma.

Vivuko hivyo vilivyozinduliwa leo vinauwezo wa kubeba watu 240 kwa wakati mmoja kwa kasi ya dakika 5 hadi 6 hivyo uwekezaji huo unakwenda kuondoa kabisa changamoto ambayo wananchi wamekuwa wakiipata kwa kipindi kirefu.

Kwa upande wa Wakuu wa Wilaya ya Ilala na Kigamboni wamemshukuru Rais kwa juhudi zake na maono katika kuleta ustawi kwa jamii hapa nchini hususani Wilaya ya Ilala ,Kigamboni na Mkoa kwa ujumla.

Maboreho ya vivuko hivyo na uwekezaji wa vivuko vipya unaendelea sio tu Magogoni bali hata maeneo mengine ikiwemo ziwa Victoria, Tanganyika na Ziwa Nyasa.

Waliopora ardhi za Vijiji wazirudishe - Wasira
NIDA yawatahadharisha Wananchi taarifa feki mtandaoni