Makamu Mwenyekiti wa Chama Chama Mapinduzi – CCM Bara, Stephen Wassira, ameiagiza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, kuhakikisha ardhi ya vijiji iliyoporwa kinyume cha sheria, inarudishwa kwa wananchi.
Wasira alitoa maagizo hayo leo jijini Dodoma, wakati akizungumza na viongozi pamoja na wanaCCM waliojitokeza kumpokea katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM.
Alisema kuna watu wamejimilikisha ardhi kwa kutoa rushwa jambo ambalo CCM inaakataa kwa nguvu zake zote.
“Haki ya Watanzania kumiliki ardhi ni sera ya msingi kwa CCM. kuna watu wanajimilikisha maeneo makubwa na hawayaendelezi kwa kutoa rushwa. Tunaomba maeneo yote ambayo yanamilikiwa kinyume cha sheria yarudishwe kwa wananchi,” alisisitiza.
“Tunataka kuona watu wakipata matatizo sehemu yao sahihi ambayo wanaweza kupata ufumbuzi iwe CCM. Hivyo tunaendelea kuhamasisha kuwa kitu kimoja. Hii ni muhimu hasa kipindi hiki tunapoelekea katika uchaguzi mkuu, lazima tuungane ili tushinde kwa kishindo.