Na, Saulo Steven – Manyara.

Chama cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Manyara kinatarajia kufanya matembezi yenye lengo la kuunga mkono maamuzi ya Mkutano mkuu wa chama hicho Taifa, yatakayofanyika Januari 25-2025.

Akizungumizia matembezi hayo Katibu wa siasa na uenezi mkoa wa Manyara, John Nzwalile amebainisha kuwa lengo la matembezi ni kuunga mkono azimio la mkutano mkuu CCM Taifa kwa kuwachagua Dkt.Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea urais wa chama hicho kwa upande wa Jamhuri ya Muungano na Dkt. Hussein Mwinyi upande wa Zanzibar katika Uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Aidha, Nzwalile ameongeza kuwa matembezi hayo yatakayofanyika Januari 25 yataongozwa na Mwenyekiti wa Ccm mkoa wa Manyara, Peter Kiroya na kupokelewa na Mwenyekiti wa UWT Taifa, Marry Chatanda.

Sanjari na hayo muenezi huyo wa ccm mkoa wa manyara amewataka wana ccm kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa huo kujitokeza kwa wingi ,ikiwa ni pamoja na Maafisa usafirishaji (Bodaboda), Mama lishe, Baba lishe na makundi mbalimbali yamekaribishwa katika matembezi hayo.

Wanafunzi epukeni vitendo viovu - DC Mgeni
Tetesi za usajili Duniani Januari 24,2025