Kikosi maalum cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa Kushirikiana na Wananchi kinaendelea na Operesheni ya kuwatafuta na kuwaokoa Wavuvi katika Ziwa Rukwa ambapo kufikia leo Januari 25, 2015 saa tisa mchana, miili ya Wavuvi nane imepatika.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa ameyasema hayo akiwa ameambata na Waziri Wa Mifugo na Uvuvi, Dkt. Ashatu Kijaji, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Edwin Mhede.

Aidha, ametoa pole kwa Wananchi wa Nankanga na kusema kuwa kufuatia upepo mkali uliotokea mnamo tarehe 23 Januari 2025 na kuwakuta Wavuvi 550 wakiwa katika shughuli zao ambapo jitiada za awali zilifanikiwa kuwaokoa Wavuvi 540 wakiwa salama.

“Kwa taarifa tulizozipata sasa, pamoja na jitihada nzuri za mafanikio tuliyopata ya kuokoa ndugu zetu 540 ambao tumewaokoa kutoa ziwani kutokana na takwimu tulizokuwa nazo jana, lakini bahati mbaya kwa taarifa nilizo nazo sasa kutoka kwa wanaonendelea ukoaji ziwani tumewapoteza ndugu zetu saba” ameeleza Bashungwa saa sita mchana.

Bashungwa ameeleza zoezi za ukoaji linaendelea likiongozwa na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji CGF John Masunga ambae anatumia helkopta kuwasiliana Vikosi maalum vya uokoaji ambao wanashirikiana na Wananchi ambao wana jumla ya vyombo 19.

Bashungwa ametoa wito kwa Wananchi na Watanzania kufuatilia na kuzingatia taarifa zinatolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa kwa sababu Rais, Dkt. Samia ameiwezesha mamlaka ya Hali ya Hewa kuwa na vifaa vya kisasa vinavyotoa taarifa za uhakika kwa wakati.

Aidha, Bashungwa ameeleza kuwa Rais Dkt. Samia anaendelea kuimarisha Jeshi la zimamoto na Uokoaji ili kuteleleza majukumu yake kwa ufanisi ambapo ameliwezesha Jeshi hilo linanunuq helikopta moja ya kuokoa na kuzima moto, magari 150 ya kuzima moto, magari 40 ya kubebea wagonjwa na boti 23 za kuzima moto na uokoaji.

Kwa upande wake, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, CGF John Masunga ameeleza kuwa Oparesheni ya Ukoaji itaendelea vizuri kwa kuhakikisha wavuvi wote waliokuwa ziwani wanapatikana wakiwa hai au kupata miili yao.

GGF Masunga amesema Kikosi Maalum cha Askari cha Uokoaji kutoka Dar es salaam kitafika hapo Nankanga kuongeza nguvu ya uokozi kwa kushirikiana Kikosi na Wananchi wanaoendelea na shughuli hiyo.

Mkuu wa wilaya ya Sumbwanga Nyakia Chirukile amesema Zoezi la Wananchi kuitambua miili ya ndugu zao linafanyika katika Zahanata ya kijiji Nankanga ili kuwezesha taratibu za mazishi kufanyika.

Awali, Diwani kata ya Nankanga, Anyisile Kayuni ametoa shukrani kwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa faraja na upendo mkubwa kwa Wananchi kwa kuwaagiza Mawaziri kuja na vikosi maalum kuweka kambi na kuhakikisha ukoaji unafanyika pamoja na shughuli nyingine.

Barabara tisa DSM zafungwa kupisha mkutano wa Nishati
EPL:Ni Chelsea au Manchester City kuingia TOP FOUR leo