Katika mwaka wa fedha 2024/25, Wizara ya Ujenzi kupitia TANROADS imetenga fedha kiasi cha Shilingi bilioni 1.8 kwa ajili ya kushughulikia masuala ya Usalama Barabarani, ikiwemo kuweka na kukarabati taa za barabarani zilizoharibika kote Nchini.

Naibu waziri wa Ujenzi, Godfrey Kasekenya ameyasema hayo hii leo Januari 28, 2025 Jijini Dodoma katika mkutano wa 18 wa Bunge wakati akijibu swali la Mbunge Abdul Hafar Idrissa aliyetaka kujua ni lini Serikali itafanya ukarabati wa taa za barabarani zilizoharibika kwa kugongwa au hitilafu nyingine.

“Kwa sasa TANROADS ipo katika hatua ya manunuzi ya kuwapata wakandarasi watakaofanya kazi hiyo na Baada ya kukamilika kwa hatua ya manunuzi na wakandarasi kupatikana, kazi ya ukarabati na uwekaji wa taa hizo itafanyika kulingana na mahitaji ya kila mkoa,” amesema.

Hata hivyo amesema Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) imekuwa ikichukua hatua mbalimbali za kuboresha sehemu korofi katika barabara kama vile milima mikali, Mbuga na sehemu zenye udongo wa mfinyazi.

“Mheshimwa Spika Hatua hizo ni pamoja na ujenzi kwa kutumia zege, ujenzi kwa kutumia mawe  Pamoja na kuzingatia mahitaji lakini pia uamuzi wa ujenzi wa aina gani utatumika kuzingatia gharama za upatikanaji wa mali ghafi za ujenzi zinazopatikana kwa urahisi katika eneo husika,” amesema Kasekenya.

Huduma ya umeme Afrika kuwafikia watu Mil. 300 - Dkt. Adesina
Kauli ya udhalilishaji: LHRC yataka RC Chalamila awajibishwe