Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika – AfDB, Dkt. Akinumwi Adesina amesema Benki ya Maendeleo ya Afrika na Benki ya Dunia zimetengeneza njia iliyo wazi ya kufikia lengo la upatikanaji wa huduma ya umeme barani Afrika kwa watu Milioni 300.
Dkt. Adesina ameyasema hayo hii leo Januari 28, 2025 katika Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi za Afrika ulioingia katika siku yake ya pili na unaofanyika jijini Dar es Salaam.
Amesema, “Benki ya Maendeleo ya Afrika na Benki ya Dunia zimetengeneza njia iliyo wazi kabisa ya kufikia lengo la upatikanaji wa huduma ya umeme Afrika kwa watu milioni 300.”
Aidha, Rais huyo wa AfDB ameongeza kuwa, Benki ya Maendeleo ya Afrika na Benki ya Dunia zitatoa dola bilioni 40 (TZS trilioni 102) ili kufanikisha lengo hilo.