Rais wa Benki ya Dunia (WB), Ajay Banga amesema katika muongo ujao, Vijana milioni 360 wa Afrika watakuwa tayari kuingia kwenye soko la ajira kipindi ambacho pia mfumo wa Afrika unatarajiwa kutoa ajira kwa vijana milioni 250.

Banga ameyasema hayo hii leo Januari 28, 2025 katika Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi za Afrika ulioingia katika siku yake ya pili na unaofanyika jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa kipindi hicho pia kitawaacha vijana watatu kati ya watano, bila fursa ya kazi inayowapa kipato na heshima.

Amesema, “ili Afrika ifaidike, sote tunahitaji kubadili mtazamo huu, kwa sababu makadirio si hatima. Tunaweza kubadili hali hii na kuwasaidia hao vijana watatu kati ya watano.

Rais huyo wa WB pia amesema safari za mafanikio zinaendeshwa kwa matumaini, lakini uhalisia unatimizwa kwa vitendo.

Tanga: Wahalifu, Wavuvi haramu wakalia kuti kavu
Mpango wa Kitaifa wa Nishati kuzinduliwa - Dkt. Samia