YALIYOJIRI LEO JANUARI 28, 2025 MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA KUHUSU NISHATI ULIOFANYIKA JNICC JIJINI DAR ES SALAAM UMETAMATIKA.

Zifuatazo ni baadhi ya nukuu za Rais na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dkt. Akinwumi Adesina

1. Napenda kutoa shukrani zangu kwa Rais Samia Suluhu Hassan, kwa ukarimu wake mkubwa wa kutukaribisha kwa ajili ya Mkutano huu, Wewe ni kiongozi wa kipekee! Daima ni furaha kubwa kuwa Tanzania!

2. Napenda pia kutoa shukrani zetu kwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Rais Ghazouani, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Mauritania, kwa kushirikiana nasi katika kuandaa Mkutano huu.

3. Ninawashukuru sana, Marais na Wakuu wa Serikali, kwa kuitikia mwaliko wetu na kwa kuja kwa idadi kubwa isiyo ya kawaida. Hii inaonesha umuhimu wa juu na dhamira ya kisiasa mnayoweka katika kupanua upatikanaji wa umeme kwa wananchi wenu.

4. Upatikanaji wa umeme ni muhimu kwa ukuaji wa kiuchumi wa Afrika, Ukosefu wa umeme wa kutosha hupunguza Pato la Taifa (GDP) la Afrika kwa asilimia 2 hadi 4 kila mwaka.

5. Viongozi, tangu Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) ilipozindua Mpango wa Nishati Mpya kwa Afrika mwaka 2016, mwanzoni mwa muhula wangu wa kwanza kama Rais wake, maendeleo makubwa yamepatikana katika kupanua upatikanaji wa umeme, asilimia ya watu waliopata umeme barani Afrika imeongezeka kutoka 39% mwaka 2015 hadi 52% mwaka 2024.

6. Benki ya Maendeleo ya Afrika imewezesha zaidi ya watu milioni 25 kupata umeme, hata hivyo, licha ya maendeleo haya, Afrika bado ina watu milioni 571 wasiokuwa na umeme, sawa na asilimia 83 ya watu wote duniani wasio na umeme, zaidi ya watu bilioni 1 hawana ufumbuzi wa kupikia kwa usafi, hali ambayo inaathiri vibaya afya ya wanawake, watoto, na maisha yao.

7. Sasa ni wakati wa kuchukua hatua madhubuti kupunguza idadi hizi zaidi, ndiyo maana mimi, pamoja na Ajay Banga, Rais wa Benki ya Dunia, tulishirikiana kuzindua Mission 300, lengo likiwa ni kupanua upatikanaji wa umeme kwa watu milioni 300 barani Afrika ifikapo mwaka 2030.

8. Misheni 300 imekua na kuwa harakati ya kimataifa, tukiungwa mkono na Tume ya Umoja wa Afrika na washirika mbalimbali.

Usambazaji Mitungi ya Gesi yawafikisha REA Kilimanjaro 
Bungeni: Pori la akiba Pande fursa ya uwekezaji DSM - Kitandula