Tanzania na Somalia zimesaini mikataba miwili ya makubaliano ya kushirikiana na katika masuala ya Ulinzi na Usalama pamoja na kubadilishana Wafungwa.
Mikataba hiyo, imesainiwa Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Somalia, Balozi Ahmed Moalim Fiqi.