Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Simiyu, Latipha Juma (17), mkazi wa Kata ya Kidinda Wilayani Bariadi mkoani Simiyu amefaruki kwa kujinyonga akitumia mtandio chumbani kwake, usiku wa kuamkia Januari 30 2025
Akizungumza na Waandishi wa Habari, mama mzazi wa binti huyo, Happines Lushiba ambaye alimkuta mwanae akiwa amejinyonga asubuhi alipokuwa akimwamsha kwenda shule, amesema Latipha hakuwa na tatizo lolote na walikuwa naye hadi walipoachana kwenda kulala usiku.
Amesema, anachokumbuka binti yake alihitaji kushonewa sare mpya za shule andapo angefaulu mtihani wa kidato cha pili, lakiji cha kushangaza licha ya kutimiza ahadi yake hiyo kabla bado hakumwambia kama kuna changamoto nyingine iliyokuwa ikimsumbua kiasi cha kufikia maamuzi hayo.
Amesema, “aliniambia nimshonee nguo za shule na nikafanya hivyo alikwenda shule akiwa amependeza sana lakini sijui alikuwa na shida gani angeniambia tu maana nimekwenda kumuamsha asubuhi awahi shule nakuta tayari amejinyonga.”
Akirhihitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda Polisi Mkoa wa Simiyu, Edith Swebe amesema wataendelea kufuatilia, ili kujua chanzo cha tukio hilo na kutoa wito kwa jamii kujenga ukaribu na Watoto na kuzungumza nao, ili kujua changamoto zinazowakabili.