Mitambo nane katu ya tisa ya kuzalisha umeme katika mradi wa bwawa la Mwalimu Nyerere (JNHPP) tayari imekabidhiwa kwa Serikali baada ya kuwashwa.
Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko Bungeni jijini Dodoma na kuongeza kuwa imebakia mashine moja ambayo itakuwa tayari mwishoni mwa mwezi Februari 2025.
Aidha, ametaja ongezeko la wadau ambao wako tayari kwa ajili ya kuboresha upatikanaji wa umeme Afrika na kupelekea Benki ya Dunia kutoa ahadi ya dola za kimarekani bilioni 22.
Wadau hao ni pamoja na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) dola bilioni 18.2, Benki ya Maendeleo ya Kiislamu dola bilioni 2.7, Benki ya Maendeleo ya Asia dola bilioni 1.5 na Benki ya Maendeleo ya Ufaransa dola bilioni 1.