Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa(Takukuru) Mkoa wa Mwanza katika kipindi cha Oktoba hadi Disemba imefuatilia utekelezaji wa miradi 13 ya maendeleo inayohusisha sekta ya Elimu, Biashara na Barabara yenye thamani ya zaidi ya shilingi Billioni 4.4
Akizungumza na vyombo vya habari Kaimu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mwanza, Idrisa Kisaka amesema katika miradi hiyo yenye thamani ya zaidi ya Bilioni 4, iliyokutwa na mapungufu ilitolewa mapendekezo juu ya namna bora ya kuiboresha.
Ufuatiliaji huo, umesaidia utekelezaji wa mapendekezo kwa zaidi ya asilimia 65.2 na kupeleka miradi hiyo kuwa na ubora kwa kiwango kilichokusudiwa.

Katika kipindi cha Januari hadi Desemba 2024,Takukuru Mkoa wa mwanza imefanikiwa kudhibiti kiasi cha shilingi millioni 366.9 kwenye ukusanyaji kodi ya zuio TRA pamoja na kwenye mnada wa mifugo Misungwi.
Pia Kisaka amewaomba wananchi wa mkoa wa Mwanza kuendelea kushirikiana na taasisi hiyo katika kuzuia vitendo vya rushwa kwenye maeneo yote ya utoaji wa huduma,kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika kwenye zoezi zima la uchaguzi.
Aidha, amewaomba wadau wote wanaotoa huduma waendelee kuunga mkono mapambano dhidi ya rushwa kupitia program ya Takukuru Rafiki kwa kutatua kero za wananchi kwa wakati.