Aston Villa imetangaza rasmi kumsajili kwa mkopo Marcus Rashford kutoka . Mshambulizi huyo Mwingereza mwenye umri wa miaka 27 anajiunga na klabu ya Birmingham hadi mwisho wa msimu wa sasa.
Rashford, ambaye ameichezea timu ya taifa ya Uingereza mara 60 na kufunga mabao 17, ni zao la akademi ya Mashetani Wekundu. Amecheza zaidi ya mechi 400 kwenye kikosi cha kwanza cha Manchester United, akifumania nyavu mara 138, na ameisaidia klabu hiyo kupata Ligi ya Europa, Vikombe viwili vya FA na Vikombe viwili vya Ligi.
Fowadi hodari ana uwezo wa kucheza katika nafasi yoyote ya ushambuliaji. Kuhamia kwake Aston Villa kunaashiria uzoefu wake wa kwanza wa kucheza katika klabu tofauti ya Uingereza.
Rashford anaweza kucheza kwa mara ya kwanza kwa timu yake mpya mnamo Februari 9 katika mechi ya Kombe la FA dhidi ya Tottenham.
Siri imefichuka
Kwa wajuzi wa Mambo tunaamini Rashford amekuwa na shauku ya kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa msimu huu na hilo lilikuwa linawezekana nje ya United.Unoted wanashiriki michuano ya Europa msimu huu. Astonvilla ni moja ya timu 8 zilizofuzu moja kwa moja hatua ya 16 bora za Ligi ya mabingwa ulaya na Rashford atashiriki michuano hiyo msimu huu mara baada ya kujiunga. Uwepo wake utaongeza ubora wa Aston villa na kuifanya timu hiyo kufika mbali kwenye michuano hiyo.
Kumbe Ishu ya Barcelona ilikuwa geresha tu
Sikuwahi kumsikia Laporta raisi wa Barcelona akisema mahali popote kwamba anamtaka Rashford kwa mkopo na sidhani kama Kocha Hans Flick amekuwa akivutiwa na mwenendo wa Rashford kwa msimu huu ikizingatiwa eneo lake la ushambuliaji limekamilika kwa kuwa na watu kama Lewandowski,Rafinha,Lamine Yamal,Dejong na wengine wengi ambao ukiwalinganisha na Rashford ni bora zaidi yake.
Lakini pia ishu ya Barcelona kutosapata wasaa wa kufanya usajili wowote msimu huu ungekuwa kikwazo kwa wacatalunya hao .Iliwalazimu kumwacha Dani Olmo kwa sababu sheria ziliwabana ingewezekana vipi kumsajili Rashford.
Sote tunaamini Rashford kwenda Barcelona msimu huu ni ndoto za abunuasi na kilichofanyika ni kumfanyia promo thamani yake ipatikane ili apate timu yoypte inayoshiriki ligi ya mabingwa ulaya.