Mawakala wa vyama vya siasa katika uboreshaji wa Daftari la Wapiga kura nchini wametakiwa kutoingilia utekelezaji wa Watekelezaji wa majukumu ya waandikishaji wa Wapiga kura katika Daftari la kudumu la Wapiga kura vituoni. Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Rufaa Mstaafu Mbarouk S. Mbarouk wakati akifungua mafunzo ya uboreshaji wa Daftari la kudumu la Wapiga kura wa mkoa wa Pwani huko Kibaha ambapo watendaji wa tume ya uchaguzi kutoka halmashauri ya Tisa za mkoa huo. Amesema, Mawakala wa Vyama vya siasa wakati wa uboreshaji wa Daftari la kudumu la Wapiga kura hawatakiwi kuingilia utendaji wa Waandikishaji vituoni.
Jaji Mbarouk amesema maelekezo zaidi ya kuhusu mawakala wa vyama vya siasa yatatolewa na wakufunzi na ni muhimu kuyazingatia na kwamba Mawakala hao wataruhusiwa kuwepo katika vituo vya kuandikisha Wapiga kura wakati wa uboreshaji wa Daftari la kudumu la Wapiga kura lakini si kuingilia utendaji kazi wao. Amesema, ”jambo hili ni muhimu kwani litasaidia kuleta uwazi katika zoezi zima kwani pia mawakala hao watasaidia kutambua waombaji wa eneo husika hivyo kupunguza kutokea kwa vurugu zisizokuwa na lazima” Aidha, Mbarouk amesema Tume imetoa kibali cha kutoa elimu ya mpiga kura wakati wa uboreshaji wa Daftari kwa asasi za kiraia 157 na asasi za kiraia 33 kwa ajili ya uangalizi wa zoezi hilo.
”Ni muhimu kutoa ushirikiano kwa asasi hizo zitakapofika kwenye maeneo yenu kwaajili ya kutekeleza majukumu yao ambapo Tume itawapa vitambulisho kwa urahisi wa kuwatambua,” amesema Jaji Mstaafu Mbarouk. Afisa Uandikishaji wa Wilaya ya Mkuranga, Waziri Kombo amesema Wilaya hiyo imeandaa vituo 578 vya waboreshaji wa Daftari la kudumu la Wapiga kura ikiwa ni kwa lengo la kuwafikia wananchi. Amesema, vifaa vya uboreshaji wa Daftari la kudumu la Wapiga kura awamu hii vimeboreshwa ambapo mwananchi ataweza kujiandikisha kwenye kata au wilaya kwani kujiandikisha ni haki kwa kila mpiga kura.
Naye Afisa Uandikishaji wa Daftari la kudumu la Wapiga kura Wilaya ya Kibaha, Adinani Livamba amesema uboreshaji wa Daftari la kudumu la Wapiga kura hilo ni kwa waliofikia umri wa miaka 18 wa kupiga kura mwaka huu na wale ambao wanataka kubadilisha taarifa hasa waliohama makazi kutoka sehemu walikojiandikisha awali. Kwa upande wake Afisa Uandikishaji wa Daftari la kudumu la Wapiga kura Halmashauri ya Chalinze, Archanus Kilaji amesema mafunzo hayo yatawasidia kujifunza kutumia mitambo ya kuboresha Daftari la Wapiga kura kwani mitambo yake ni aina mpya kabisa.

Azma ya Serikali ni kuhakikisha Wananchi wanapata Umeme wa uhakika - Kapinga
Maamuzi ya CAF yawaumiza Simba robo fainali Shirikisho