Manchester United bado iko tayari kumuuza winga wa Argentina Alejandro Garnacho, 20, na kiungo wa kati wa Uingereza Kobbie Mainoo, 19, msimu wa kiangazi (Guardian)

Mshambulizi wa Brazil Matheus Cunha, 25, ana nia ya kuhamia klabu kubwa licha ya kusaini mkataba mpya wa Wolves . (Football Insider)

Nottingham Forest ilikataa ofa ya siku ya mwisho kutoka kwa Chelsea kwa mlinzi wa Brazil Murillo, 22. Ingekuwa mauzo ya rekodi ya klabu. (Telegraph – Subscription required )

Mshambulizi wa Manchester United na Uingereza Marcus Rashford, 27, alikataa kuhamia klabu moja ya Uturuki kabla ya kujiunga na Aston Villa kwa mkopo. (Manchester Evening News )

Rashford anaweza kupoteza kama 100% ya pesa za udhamini anazopokea kutoka kwa Nike kwasababu kampuni hiyo kubwa ya mavazi ya michezo inaichukulia Aston Villa kama kitengo cha chini cha klabu kuliko United . Nike pia inaweza kumuomba alipe kiasi cha ada za kusaini. (Mail Plus -Subscription required)

Wachambuzi wa wanaamini kuwa inaweza kufika hadi mwaka 2032 kabla ya Old Trafford kujengwa upya kikamilifu au kuendelezwa upya. (Mail Plus – Subscription required)

g

Chanzo cha picha,Getty Images

Maelezo ya picha,Nico Gonzalez

Barcelona haikupokea pauni milioni 8.5 kutokana na mauzo ya kiungo wa kati wa Porto Muhispania Nico Gonzalez, 23, kwenda Manchester City , kwasababu klabu hiyo ya Ureno ililipa klabu hiyo ya Catalan ada ya pauni milioni 2.5 ili kupunguza nusu ya kipengele cha mauzo. (ESPN)

Newcastle United wanaegemea kujenga uwanja mpya karibu na St James’ Park. (Telegraph – Subscription required)

United wanataka kukataa ofa ya mkopo ya Benfica kwa ajili ya mlinzi wa Uholanzi Tyrell Malacia, 25, ili kuashiria mwisho wao kuwaondoa wachezaji kwa masharti yasiyofaa. (Mail Plus – Subscription required)

Miaka 40 ya Cristiano Ronaldo kutoka ufukara mpaka kutajirika
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Februari 5, 2025