Steven Gerrard yuko mbioni kushika usukani wa Carlisle United, klabu inayoshiriki ligi daraja la nne la soka la Uingereza kwa sasa. Habari hii inatoka kwa Mail Sport.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, umiliki wa klabu hiyo kutoka Marekani unazingatia kwa dhati umahili wa Gerrard kufuatia kutimuliwa kwa Mike Williamson. Nafasi ya mwisho ya Gerrard ya ukocha ilikuwa Saudi Arabia, ambapo aliiongoza Al-Ettifaq tangu msimu wa joto wa 2023 kabla ya kuachia ngazi mwishoni mwa Januari 2025.

Kwa muktadha, Carlisle United inashiriki Ligi ya Pili, daraja la nne la kandanda ya Uingereza, na kwa sasa iko mkiani mwa jedwali katika nafasi ya 24.

Makala: Valentine ya Mwanaume kupiga magoti
Real Madrid watoa neno Birthday ya Ronaldo