Prince Karim Al-Hussaini, Aga Khan IV na Imamu wa 49 wa Kishia Ismailia amefariki dunia jijini Lisbon, akiwa na umri wa miaka 88 ambapo kifo chake kimethibitishwa na Mtandao wake wa Maendeleo wa Aga Khan katika chapisho la X, tovuti ya mtandao wa kijamii.

Aga Khan, ambaye ni mmoja wa watu tajiri zaidi duniani ambaye alikuwa kiongozi wa kiroho na mfadhili, alianzisha Wakfu wa Aga Khan mnamo mwaka 1967, ili kuleta pamoja misaada ya kibinadamu, kifedha na kitaalamu kwa lengo la kukabiliana na changamoto zinazowakabili watu maskini duniani.

Wakfu huu unafanya kazi katika nchi 18 barani Afrika, Asia, Ulaya, Mashariki ya Kati na Amerika Kaskazini na taarifa imesema, Uongozi, Wafanyakazi na wanaojitolea wa Wakfu wa Aga Khan wanatoa rambirambi zao kwa familia na jamii ya Ismailia duniani.

 

Aga Khan Prince Karim al-Hussaini akiwa na Prince William na Princess Kate mwaka 2019 (Picha ya Getty Images)

Katika salam zake za rambirambi, Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amemtaja Aga Khan kama “ishara ya amani, uvumilivu na huruma katika ulimwengu wetu wenye matatizo” kufuatia kifo cha kiongozi huyo wa kidini.

Malala Yousafzai, mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel na mwanaharakati wa elimu, alisema urithi wake “utaendelea kupitia kazi ya ajabu aliyoongoza kwa elimu, afya na maendeleo duniani kote”.

Alizaliwa huko Geneva Desemba 13, 1936 na alikulia nchini Kenya. Baadaye alirejea Uswizi, akihudhuria Shule ya kipekee ya Le Rosey kabla ya kwenda Marekani kusoma historia ya Kiislamu katika chuo cha Harvard.

Ramovic hakupaswa kuondoka Yanga,Huyu mpya anarekodi mbovu Tanzania
Waarabu wajipanga kumwaga milioni 900 kumnasa Kibu Denis