Klabu ya Yanga imetangaza kuvunja mkataba na aliyekuwa kocha wake mkuu Saed Ramovic na kumtambulisha kocha mpya Miloud Hamdi aliyetokea Singida Black Stars.

Huu ni mwanzo mpya kwa Yanga katika harakati za kutetea makombe Yake waliyoyatwaa msimu wa 2023/24. Wengi wanaamini mwenendo wa kiuchezaji wa Ramovic haukuwaridhisha viongozi wa Yanga kitu ambacho si kweli.

Tutafakari kidogo

Yanga walimuajiri Ramovic November 15 akichukua nafasi ya Miguel Gamondi aliyetimuliwa baada ya kupoteza michezo miwili mfululizo  ya Azam FC bao 1-0 na Tabora United mabao 3-1.

Ramovic amehudumu ndani ya Yanga kwa miezi miwili na siku 21 na katika siku hizo amewaongoza Yanga kucheza michezo 12 akishinda michezo 8 sare 2 na kupoteza michezo 2.

Yanga chini ya Ramovic haijapoteza wala kupata Sare kwenye michezo ya ligi kuu ya NBC zaidi aliimarisha Safi za ushambuliaji kwa kufunga mabao 22 na kufungwa mabao mawili pekee katika mechi 6.

Binafsi nilimuona ni kocha sahihi kwa Yanga hasa kipindi hichi ambacho baadhi ya Wachezaji wamekuwa wakikumbwa na majeraha ya mara kwa mara na baadhi yao kutokuwa na kiwango cha awali.

Mfano ni namna alivyowatumia Wachezaji tofauti na wale waliozoeleka kwenye mchezo wa CRDB CUP na kuibuka na ushindi mnono wa 5-0 dhidi ya Copco. Lengo la Ramovic ilikuwa ni kuondoa utegemezi wa mchezaji mmoja mmoja na kutengeneza timu inayoweza kucheza kwa kiwango kilekile anapokosekana mchezaji husika.

Enzi za Ramovic Wachezaji wote walikuwa Sawa mbele ya macho yake na hakusita kuwaweka benchi Wachezaji vinara kama Aziz ki,chama,pacome na hata maxi nzengeli na timu iliendeleea kufanya vyema.

CV ya Miloud Hamdi ni kubwa nje ya Tanzani ila hapa kwetu amechemka 

NI kocha mwenye CV kubwa kwa soka la Africa na Yanga watanufaika naye kama watampa nafasi Yake pasipo kumuingilia katika majukumu Yake. Kocha huyu si mgeni na soka la Tanzania ,ameshawahi kuwanoa Singida Black Stars msimu huu akichukua nafasi ya Patrick Aussems aliyetimka klabuni hapo Novemba 24 ,mwaka 2024.

Kocha Miloud Hamdi alitangazwa rasmi Novemba 30 kuwa kocha wa Singida Black Stars na aliiongoza Singida black stars katika michezo 4 àkishinda mchezo 1 pekee dhidi ya Coastal Union kwa mabao 3-2 na kupoteza michezo mitatu dhidi ya Azam FC mabao 2-0, Namungo 2-1 na Yanga 5-0. Kwa manen mengine kocha huyu ameokota alama tatu pekee kati ya 12 alizokuwa anazipigania akifungwa mabao 11 na kufunga mabao 3 pekee katika mechi hizo 4.Hamdi ana cv nzuri nje ya Tanzania lakini amechemka Tanzania.Leo anaiongoza Yanga kucheza dhidi ya Ken Gold ataweza kufanya muujiza?

 

CAG apongeza kasi ujenzi wa Uwanja wa Ndege Msalato
Tanzia: Kiongozi Aga Khan wa IV ametangulia