Jimbo la Newala Vijijini limeendelea kunufaika na Miradi ya Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), ambapo Agosti 30, 2022 Serikali iliingia makubaliano na kampuni moja ya simu kujenga mnara katika Kata ya Chitekete kupitia mradi wa Mipakani na Maeneo Maalum wa awamu ya sita (BSZ PH6), ambao ulikamilika na Wananchi wananufaika na huduma.

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya habari, Maryprisca Mahundi ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Newala Vijijini, Maimuna Mtanda ambaye aliuliza Je, ni lini Serikali itajenga minara ya simu katika maeneombalimbali ya jimbo la Newala vijijini yenye changamoto ya mawasiliano.

“Aidha kupitia mradi wa Tanzania ya Kidigitali Awamu ya Kwanza (DTP PH1) ambao mkataba wake ulisainiwa tarehe 13 Mei, 2023, Kata ya Makukwe katika Jimbo la Newala Vijijini, ilijumlishwa na kupata mtoa huduma kampuniya Yas na kwasasa wamepata kibali cha ujenzi na Mkandarasi anajiandaakwenda kuanza ujenzi wa mnara huo.”

Hata hivyo, amesema Serikali kupitia UCSAF, itafanya tathmini katika maeneo mbalimbali ya Jimbo la Newala vjijini ili kubaini maeneo yenye changamoto ya mawasiliano ya simu.

“Tutafanya tathmini kama alivyowasilisha Mhe. Mbunge ili kubaini mahitaji halisi na kuyaingiza katika mpango wa kuyafikishia huduma katika utekelezaji wa miradi ijayo ya mawasiliano ya simu kulingana na upatikanaji wa fedha.”

Vilevile amesema Serikali imepanga kufikisha mkongo wa taifa mashuleni mpaka kufikia Desemba 2025 iwe imeweza kufikiwa.

Ujenzi Kituo cha kupoza Umeme Urambo umekamilika - Kapinga
Mfumo wa Stakabadhi Ghalani kuimarishwa Nchini