Serikali kupitia Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA), Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) na Mamlaka ya Udhibiti Ubora wa Mbolea Tanzania (TFRA) imeweka mikakati ya kudhibiti uingizaji wa pembejeo feki za mazao, ili kuwasaidia wakulima wasipate hasara. Naibu Waziri wa Kilimo, David Silinde ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mbunge Viti Maalum, Neema Mwandambila ambaye aliuliza Je, ni Mkakati upi Serikali imeuweka Ili kudhibiti uingizaji wa pembejeo feki. Akijibu swali hilo Silinde amesema, “Ili kudhibiti uingizaji wa pembejeo feki za mazao nchini Serikali imeweka mkakati wa Kutambua na kusajili waagizaji wote wa pembejeo nchini ili kudhibiti uingizaji holela wa pembejeo nchini,Kufanya ukaguzi wa kila shehena ya pembejeo za kilimo inapofika bandarini au mpakani na kuchukua sampuli kwa ajili ya uchambuzi wa kimaabara.”
Aidha ameongeza kuwa, “kutoa elimu kwa wakulima na wauzaji wa pembejeo za kilimo kuhusu utambuzi wa pembejeo feki, utunzaji na matumizi bora ya pembejeo na Kufanya kaguzi za mara kwa mara katika maghala na maduka ya pembejeo na kuchukua hatua stahiki kwa wahusika ikiwemo kuwafutia leseni za kuuza pembejeo zote wale wote wanaobainika kuuza au kusambaza pembejeo feki.” Hata hivyo, Silinde amesema Serikali kupitia mawakala wametoa fursa kwa wafanya biashara wote wanaotaka kuingia katika biasahara ya mbegu pamoja na mbolea kujisajili TFRA ili kupewa kıbali cha kuuza mbolea. “Hii ni kibali cha kila mtu ambae anahitaji kufanya hiyo biashara, kwaio niseme tu kwamba wale wote wanaotaka kufanya hiyo biasahara waje na sisi tutawapa hiyo ruhusu ya kufanya biashara hiyo,” aliongeza.

Butondo aikumbusha Serikali usikivu wa Radio kwa Wanakishapu
Ujenzi Kituo cha kupoza Umeme Urambo umekamilika - Kapinga