Mbunge wa Kishapu, Boniface Butondo ameiomba Serikali kurejesha usikivu mzuri wa TBC FM radio, Ili Wananchi wapate habari za uhakika kutoka radio hiyo.

Butondo ametoa kauli hiyo Leo Februari 7, 2025 Bungeni jijini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na majibu.

“Hali ya uskifu wa TBC FM katika wilaya ya Kishapu ni ya chini sana ,Serikali Ina mpango gani kuhakikisha kwamba wananchi wa Kishapu wanaendelea kupata taarifa za uhakika kutoka TBC Radio,” amehoji Butondo.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Maryprisca Maundi amesema Serikali imelipokea suala Hilo kwa ajili ya kuzifanyia kazi kwa kutuma wataalam kwenda kuona namna ya kuboresha mnara kwa ajili ya kurejesha mawasiliano ya TBC FM yaweze kupatikana vizuri.

Madini: Utafiti kuboresha Mazingira ya Biashara Nchini
Serikali yaweka mikakati kudhibiti uingizaji Mbolea feki