Mkazi wa Kijiji cha Nyehunge, Nicholaus Paulo Kidoganya (21), amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela na Mahakama ya Wilaya Sengerema Mkoani Mwanza baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka mtoto wa miaka mitano.
Mshtakiwa huyo anadaiwa kuwa alitenda kosa hilo Desemba 23, 2024, katika Kijiji cha Nyamadoke, kilichopo Wilaya ya Sengerema, kinyume na vifungu vya 130(1)(2)(a) pamoja na kifungu cha 131(3) cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 marejeo ya mwaka 2022.
Awali, taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi ilieleza kuwa baada ya mtuhumiwa kufikishwa Mahakamani na kusomewa shtaka hilo, kwa hiari yake bila kuisumbua mahakama alikiri kutenda kosa hilo.
Alisema, siku ya tukio alimshawishi mtoto huyo kwa kumhahidi kumpa maembe yaliyokuwa juu ya mti uliokuwa kw