Dawa za kufubaza makali ya Virusi vya Ukimwi (ARV), zinapatikana bure, haziuzwi na zipo za kutosha, hivyo watumiaji hawana sababu ya kuwa na wasiwasi kuhusu upatikanaji wake.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Afya hii leo Februari 8, 2025 imeeleza kuwa imebaini uwepo wa taarifa za upotoshaji kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya Habari vinavyoelezea uhaba wa dawa hizo nchini.