Fountain Gate Foundation kupitia Mradi wa Uwezeshaji wa Maureen Memorial ukiongozwa na Mwenyekiti ambaye pia ni Rais wa Fountain Gate Academy Tanzania, Japhet Mboto Makau asubuhi ya leo wametembelea Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Babati kwa lengo la kutoa zawadi kwa Watoto wote waliozaliwa siku ya Jana tarehe 07/02/2025 katika Hospitali hiyo.

Msafara huo, umejumuisha Viongozi Mbalimbali, Wafanyakazi na Wazazi wa Fountain Gate Academy pamoja na Marafiki ukilenga kuenzi utumishi wa Hayati Maureen katika Hospitali ya Mrara na kuonesha upendo wa pekee kwa Watoto waliozaliwa Februari 7 tarehe ambayo aliyozaliwa Hayati Maureen Makau.

Katika siku hiyo, aliambatana na Watoto wake, akiwemo Rais Japhet Mboto Makau wa Fountain Gate Academy, Wendo Phares Makau na Meneja wa Fountain Gate FC.

Lakini licha ya Watoto hao kuzaliwa tarehe moja na Hayati pia walipata shuhuda za huduma aliyokuwa akiitoa katika Hospitali hiyo ambayo alifanya kazi kwa takribani miaka 14.

Baada ya Utoaji wa zawadi, msafara wote ulielekea katika Shule ya Awali na Msingi Fountain Gate Manyara kwa ajili ya chakula cha pamoja.

ARV zipo za kutosha, puuzeni taarifa za uzushi - Wizara