Arsenal na Tottenham wote wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa Fiorentina na Italia Moise Kean mwenye umri wa miaka 24. (Nicolo Schira)

Manchester United na Aston Villa zote zilikuwa tayari kutoa euro 70m (£58.3m) kwa Fermin Lopez wa Barcelona mwezi Januari, lakini mshambuliaji huyo wa miaka 21 wa Uhispania hakutaka kuhama. (Sport – In Spanish)

Barcelona ilikataa ofa ya kumsajili mshambuliaji wa Chelsea na Ureno Joao Felix katika dirisha la uhamisho la Januari kabla ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 kusaini mkataba wa mkopo kwenda AC Milan hadi mwisho wa msimu. (Sport – In Spanish)

.

Chanzo cha picha,Getty Images

Maelezo ya picha,Joao Felix

Arsenal wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Ureno Diogo Jota, huku Liverpool wakiwa tayari kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 kwa ada sahihi kwa sababu ya idadi ya michezo ambayo amekosa kutokana na jeraha. (Anfield Watch)

Atletico Madrid wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Crystal Palace na Ufaransa Jean-Philippe Mateta, 27, ambaye mkataba wake na The Eagles utakamilika 2026. (Teamtalk)

Hata hivyo, Mmiliki wa Lyon Mmarekani John Textor, ambaye ni mwanahisa mkuu katika Crystal Palace, anataka timu yake ya Ligue 1 kuwasilisha zabuni kwa Mateta yenye thamani ya pauni milioni 50. (Sun)

.

Chanzo cha picha,Getty Images

Maelezo ya picha,Jean Phillipe Mateta

Crystal Palace wamemlenga beki wa Burnley Mfaransa Maxime Esteve, 22, na mchezaji wa kimataifa wa Uholanzi wa Middlesbrough Rav van den Berg, 20, kama mbadala wa beki wa kati wa England, 24, Marc Guehi (Sun).

Everton inalenga kuwasajili nyota chipukizi wa Uingereza kama sehemu ya mpango mpya wa usajili. (Football Insider)

Wapinzani wasiwatumie Vijana kufanya vurugu - Wasira
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Februari 10, 2025