Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira amesema ni marufuku kwa vyama upinzani kuwatumia vijana kutoka mkoani Mara kama nguvu kazi ya kufanya vurugu katika maeneo mbalimbali.

Amesema CCM inamipango mizuri kuhakikisha vijana hao wanatumia nguvu zao kujiletea maendeleo ya kiuchumi na kujikwamua dhidi ya umasikini.

Wasira aliyasema hayo jana, alipokuwa akizindua ofisi ya CCM Kata ya Nyakonga wilayani Tarime, Mkoa wa Mara.

‘Nataka niwaambie wananchi wa Tarime CHADEMA wakitaka kufanya fujo mahali popote wanakuja kuchukua vijana Tarime…wanapelekwa kufanya fujo kama majeshi ya kukodi, wakitaka kufanya fujo Mbeya wanakuja, Tarime, wakitaka kufanya fujo sehemu Tarime.

“Tunawaambia vijana wa Tarime wana mvua wana jua na Tarima panalimika, kila kitu kinaota tuwasaidie vijana wa Tarime watumie fursa zilizopo…tunawaambia CHADEMA muache kuja kuchukua vijana Tarime, sisi sio eneo la mapambano, vijana wetu sio wa kukodisha kwenda katika mapambano, nasema kama mzee wa Tarime waache kuja kuchukua vijana wa Tarime.

Wasira aliwataka vijana wasikubali kuchukuliwa na kutumika katika vurugu kwa kuwa wakienda huko hupigwa, kuumizwa na hata kupata ulemavu kisha kurudishwa Tarime wakiwa na hali mbaya.

Kwa mujibu wa Wasira, Tarime ukilinganisha na wilaya nyingine za Mkoa wa Mara ina fursa nyingi zaidi, “hapa tuna madini hapa tuna wachimbaji wadogo na tunataka wachimbaji wadogo walindwe wachimbe kwa amani, tunataka wapewe mafunzo ili wachimbe wapate manufaa kutokana na rasilimali iliyowekwa na mungu katika eneo hili.”

Makamu Mwenyekiti Wasira alisema CCM na serikali yake inataka vijana wa Tarime walime kwa kuwa wanayo ardhi wananchi wengi wa wilaya hiyo wa na ujuzi wa kufuga hivyo wanaweza kuifanya Tarime yote kuwa ya ng’ombe wa maziwa.

“Kila familia ikawa na ng’ombe wawili wawili ikatufanya tukaweza kujenga kiwanda cha maziwa na watu wa Tarime wakawa wanapata pesa moja kwa moja kila mwezi, hayo ndiyo mambo tunayoyafanya kama Chama,” alisema.

Liverpool yapigwa na kitu kizito kombe la FA
Tetesi za usajili Duniani Februari 10,2025