Mbunge wa Jimbo la Kishapu, Boniphace Butondo leo Februari 10, 2025 bungeni jijini Dodoma ameibana Serikali ieleze ni lini itapeleka fedha za dharura Wilayani Kishapu ili kufanya matengenezo ya Barabara zilizoharibiwa na mvua za Elninyo Mwaka 2023/24.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Festo Dugange amesema Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini Tanzania Wilaya ya Kishapu inao mtandao wa barabara wenye urefu wa kilomita 1024.66.

 

Amesema, Kilomita 2 ni barabara za Lami, kilomita 405.64 ni barabara za changarawe na kilomita 617.02 (km 617.02) ni barabara za udongo.

Amesema, katika mwaka 2023/24, Serikali ilifanya tathmini ya mtandao mzima wa barabara katika Wilaya hiyo ili kubaini ukubwa wa uharibifu ambapo jumla ya shilingi 2,553,415,000.00 zinahitajika ili kuzifanyia matengenezo barabara hizo.

Matajiri wa Ufaransa watangaza kumtaka Tchouameni
David Moyes afafanua kukosekana kwa Mr Bean