Taarifa zisizo rasmi zimeanza kuvuja zikimuhusisha kiungo mashughuli wa Simba Fabrice Ngoma.Nyota huyo ameanza kumezewa mate na matajiri kutoka Afrika ya Kaskazini .inasemekana wako tayari kutoa kitita cha bilioni 1 ili waweze kumnasa nyota huyo mwenye uwezo wa kipekee.
Ngoma ameingia kwenye mkondo wa kutakiwa Uarabuni baada ya Clement Mzize na Aziz ki kutakiwa huko ,Bado haijawekwa wazi ni klabu ipi inahitaji huduma yake lakini Kocha Saed Ramovic na Miguel Gamondi wamekuwa wakimfuatilia kwa kina na kuna uwezekano wakawa wamempendekeza kwenye vilabu wanavyovinoa.
Chanzo ni kocha wake wa zamani Juan Garrido
Klabu ya Al- Ittihad inatingisha soka la Afrika ikiwa na akili ya kusuka kikosi upya, imemwekea Ngoma mezani dau la Dola 500,000 (zaidi ya Sh1 bilioni) ili kumng’oa Msimbazi. ili kununua mkataba wake na Simba.
Presha ya Ngoma imekuja kufuatia Al-Ittihad kumpa ajira kocha mmoja mkubwa, Mhispaniola Juan Carlos Garrido ambaye ndiye aliyetaka Ngoma achukuliwe haraka.
Garrido aliwahi pia kufanya kazi na Ngoma mwaka wa mwisho alipokuwa kocha wa Raja Athletic ya Morocco mwaka 2019, lakini hakufanya naye kazi sana kabla ya kocha huyo mwenye misimamo kuamua kutimka.
Walibya hao wameshakubaliana kila kitu na Ngoma na sasa imebaki hatua ya Simba kumalizana nao tu ambapo mabosi wa Wekundu hao wanasita kutopokea fedha hiyo ndefu kufuatia Mkongomani huyo kubakiza miezi mitano kwenye mkataba wake.
Simba ilikuwa mezani na Ngoma ikibakiza hatua ya kumsainisha tu mkataba mpya hatua ambayo kwa sasa imemfanya Mkongomani kuyo kuwa mzito kuweka wino akiwaambia mabosi hao wasubiri kwanza.
Simba inataka kufanya biashara hiyo sasa ili ivune fedha kwenye usajili huo kuliko Ngoma kuondoka bure mwisho wa msimu.
Simba iliona mabadiliko makubwa ya Ngoma akikiwasha vikali kiasi cha kubariki uamuzi wa kocha Fadlu Davids aliyempa ukubwa wa kuwa nahodha msaidizi wa kikosi hicho.
Taarifa zaidi zinasema kuwa, muda wowote kiungo huyo anaweza kusepa kwani mabosi wa Msimbazi wamevutiwa na kiasi hicho na uamuzi wa kiungo huyo kuwagomea mkataba mpya ili wasipate hasara.
Jeuri ya kutaka kumruhusu Ngoma kuondoka, inatokana na ukweli katika kikosi cha sasa kuna wachezaji wanaomudu kucheza nafasi anayocheza Mkongoman huyo akiwamo Debora Mavambo, Mzamir Yassin, Augustine Okejepha na Yusuf Kagoma ambaye kwa sasa amekuwa akitengeneza pacha na kiungo huyo anayetakiwa Libya.