Taarifa kutoka Dodoma jiji

Siku ya Jana tar. 10/02/2025 majira ya saa 4 asubuhi Kikosi chetu Kilichokua safarini kutokea Ruangwa Mkoani Lindi Kuelekea Jijini Dar es salaam kilipata ajali ya gari Mkoani Lindi kwa kupinduka na kutumbukia Mtoni (Mto Matandu).

Ajali hiyo ilisababisha majeruhi kadhaa akiwemo mwalimu wa viungo Francis Mkanula mshambuliaji wetu Yassin Mgaza pamoja na Rajab ambae ni golikipa wa timu yetu ya vijana chini ya Miaka 20, ambapo majeruhi wote walikimbizwa katika Kituo Cha Afya Nangurukuru kwa matibabu zaidi.

Majeruhi wanaendelea vizuri na baada ya vipimo na matibabu ya awali waliruhusiwa na Kikosi chetu kiliendelea na safari na kimefanikiwa kufika Dar es salaam salama.
Tunatoa shukrani kwa Wasamalia wema waliojitokeza kufanya uokoaji eneo la tukio, Madaktari pamoja na jeshi la Polisi kitengo Cha usalama barabarani Wilaya ya Kilwa, Mkoani Lindi kwa msaada na jitihada zote walizozifanya kuhakikisha kila kitu kinakua sawa.
Aidha tunavishukuru vyombo vya habari, wanahabari na taasisi mbalimbali zinazoendelea kutuma salamu za pole na kututia moyo katika kipindi hiki kigumu.

Tunawaombea Majeruhi wote wapone haraka ili waweze kurejea kwenye majukumu yao.

Maambukizi mapya ya Ukimwi kuongezeka maradufu - Byanyima
Askari 13 wanaswa na TAKUKURU Burigi, watatu waachishwa kazi