Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Daniel Sillo ametoa wito kwa Madereva wote wanaoendesha pikipiki Nchini kuzingatia Sheria ya Usalama barabarani, ili kupunguza ajali zinazoathiri Wananchi wengi na kupunguza nguvu kazi katika Taifa letu. Sillo emeyasema hayo leo Februari 11,2025 Bungeni hapa Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti malum CCM, Fatma Toufiq aliyehoji ni wananchi wangapi wamepoteza maisha kutokana na ajali za pikipiki kati ya mwaka 2022-2024. “katika kipindi cha kuanzia mwaka 2022-2024 jumla ya wananchi 1,113 wamepoteza maisha kutokana na ajali zilizosababishwa na pikipiki kwa mchanganuo ufuatao:, madereva wa pikipiki waliopata ajali na kufariki 759, abiria waliopanda pikipiki na kupata ajali zilizosababisha vifo vyao ni 283 na wananchi waliokuwa wanatembea kwa miguu kandokando ya barabara au njiani, ama walikuwa wanavuka barabara na kupata ajali ya kugongwa na pikipiki na kufariki dunia ni 71,” amesema.
Aidha, akijibu swali la nyongeza la Mbunge huyo kuhusu mkakati wa Serikali wa kuzuia vifo hivyo vinavyotokea visiendelee, Sillo ameendelea kutoa wito kwa makamanda wa usalama barabarani kuendelea kusimamia sheria za usalama barabarani pamoja na madereva, abiria na watembea kwa miguu wote kuhakikisha wanazifuata. “Kuhusu suala la abiria kupanda pikipiki zaidi ya mmoja, nielekeze kwanza makamanda wa polisi wa usalama barabarani kuzingatia na kusimamia sheria laikini pili wadau wote watembea kwa miguu na abiria wote tusikubali kupanda pikipiki zaidi ya mmoja kwahiyo kila mmoja achukue hatua za tahadhari kuhakikisha kwamba mnakuwa salama kwani mnapopanda zaidi ya mmoja ikitokea ajali wote mnafariki,” amesema.

TANESCO, EWURA imeweka mwongozo wa gharama za kuunganisha Umeme - Kapinga
Maambukizi mapya ya Ukimwi kuongezeka maradufu - Byanyima