Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir Mayardit amewafuta kazi Makamu wa Rais, James Wani Igga na Hussein Abdelbagi pamoja na Mkuu wa Usalama wa Taifa, Akech Tong Aleu na kumteua Benjamin Bol Mel kuchukua nafasi ya Wani Igga kama makamu wa rais anayewakilisha chama tawala cha Sudan People’s Liberation Movement (SPLM).

Aidha, Mwenyekiti wa Muungano wa Upinzani wa Sudan Kusini (SSOA), Josephine Lago Yang ameteuliwa kuchukua nafasi ya Abdelbagi, ambaye alishikilia wadhifa huo tangu mwaka 2020, chini ya masharti ya uimarishwaji wa makubaliano ya amani.

Kiir pia amemteuwa aliyekuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Huduma ya Usalama wa Kitaifa, Charles Chiech Meya kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, huku Wani Igga akiteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa chama Tawala cha SPLM baada ya kuondolewa kama Makamu wa Rais.

Sudan Kusini ina Makamu wa Rais watano, kufuatia muundo ulioanzishwa chini ya mkataba wa amani wa 2018, uliotiwa saini kati ya Serikali ya Rais Kiir na vikundi vya upinzani, kufuatia vita vya wenyewe kwa wenyewe na hakuna sababu rasmi iliyotolewa kuhusu kuondolewa kwa Viongozi hao wakuu wa Serikali.

India kuwekeza katika Sekta ya Nishati Nchini
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Februari 12, 2025