Arsenal, Chelsea na Liverpool wanavutiwa na mlinzi wa Bournemouth mwenye umri wa chini ya miaka 21 Dean Huijsen, ambaye ana kipengele cha kuachiliwa kwa pauni milioni 55 katika mkataba wake. (TBR Football),

Liverpool wana nia ya kumsajili winga wa England chini ya miaka 21 mzaliwa wa Ufaransa Mohamed-Ali Cho, 21, kutoka Nice. (TeamTalks)

Chelsea wanaandaa dau la pauni milioni 58.3 (euro milioni 70) msimu ujao kwa ajili ya beki wa Atletico Madrid mwenye umri wa miaka 21 Pablo Barrios. (Fichajes)

Klabu ya Saudi Pro-League Al-Nassr ilikaribia sana kufikia makubaliano ya mshambuliaji wa Uruguay Darwin Nunez kutoka Liverpool mnamo Januari kabla ya Reds kukataa mpango wa mchezaji huyo wa miaka 25. (Givemesport),Aston Villa na Arsenal wameonyesha nia ya kumsajili mshambuliaji wa Olympiakos wa Ugiriki chini ya umri wa miaka 21, 17, Charalampos Kostoulas na kiungo wa kati wa Ugiriki Christos Mouzakitis, 18. (Birmingham World)

.

Chanzo cha picha,Getty Images

Maelezo ya picha,Sir John Ratcliffe

Crystal Palace, Rangers na Norwich wanavutiwa na winga wa Birmingham Muingereza Zaid Betteka mwenye umri wa miaka 18. (Football Insider

Mmiliki mwenza wa Manchester United Sir Jim Ratcliffe anapanga kupunguza kazi zaidi ili kusaidia kuokoa pesa kwa wachezaji wapya. (Star)

Aston Villa na Paris St-Germain hazikujumuisha chaguo la kununua katika mkataba wa mkopo wa kiungo wa kati wa Uhispania Marco Asensio, 29, lakini vilabu vyote viwili viko tayari kuhama msimu ujao. (Fabrizio Romano)

Mkufunzi wa zamani wa Manchester United Erik ten Hag anaweza kuwa kwenye nafasi ya kurejea kama meneja katika klabu ya Feyenoord. (AD – Kiholanzi)

.

Chanzo cha picha,Getty Images

Roma wanataka kufanya mkataba wa kudumu na AC Milan kumnunua kiungo wa kati wa Ubelgiji Alexis Saelemaekers, 25, lakini mkataba wa kubadilishana unaohusisha mshambuliaji wa Uingereza Tammy Abraham, 27, haupo mezani. (Calciomercato – Italia)

Wachezaji wa Manchester United wanaamini kubadilika kwa mtindo wa uchezaji hadi ule unaotumiwa sasa na bosi Ruben Amorim inaweza kuwa njia bora zaidi ya kusonga mbele. (Mail)

Michezo ya Ligi ya Mabingwa, ikiwa ni pamoja na fainali, inaweza kufanyika nchini Marekani kuanzia mwaka wa 2033 na kuendelea huku Uefa ikitarajia kuingia mkataba mpya wa kimataifa wa haki za kibiashara. (Independence)

e-GA wakamilishe usanifu mfumo wa ubadilishanaji taarifa - Dkt. Mpango
Shemwelekwa ataka uzingatiaji kanuni uandikishaji Daftari la wapiga kura