Beki wa Argentina Cristian Romero anatarajiwa kupokea ofa ambayo inaweza kumfanya kuwa mchezaji anayelipwa pesa nyingi zaidi. Vyanzo vya habari vinaonyesha kuwa Spurs wako tayari kufanya juhudi kubwa kupata mchezaji ambaye wanamwona kuwa muhimu kwa malengo yao ya baadaye.
Pindi pendekezo hilo litakapowasilishwa, inabakia kuonekana kama Muargentina huyo atalikubali au badala yake ajaribiwe na mapendekezo ya klabu nyingine ambazo tayari zimeonyesha nia. Katika hali hii, ushiriki mdogo wa Tottenham katika Ligi ya Mabingwa tangu kuwasili kwa Romero unaweza kutumika kumshawishi mchezaji huyo kubadili maamuzi ya kusalia klabuni hapo na akawekeza maono yake kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Tottenham inalazimika kutumia gharama kubwa kuwanunua nyota wapya na kuwashawishi baadhi kusalia klabuni hapo kwa kuboresha mishahara yao kutokana na nafasi finyu ya Ushiriki wa Ligi ya Mabingwa ulaya kwa msimu ujao.