Ligi kuu Uingereza imeendelea tena usiku wa tarehe 12 kwa kuwakutanisha watani wa jadi wa jiji kati ya Liverpool dhidi ya Everton mchezo uliopigwa dimba la Goodson Park uwanja unaomilikiwa na Everton FC. Huu ni moja ya michezo migumu ya kuvutia katika ligi ya Uingereza na safari hii umekuja na kituko chake baada ya kadi nne nyekundu kutolewa na refarii Michael Oliver.
Tathmini ya Mchezo
Everton walikuwa wa kwanza kupata bao la Uongozi kupitia kwa Beto dakika ya 11 akimalizia pasi mpenyezo kutoka kwa Branthwaite ,bao hilo halikudumu kwan Mac Allister alisawazisha bao hilo dakika ya 16 akimalizia pasi ya Mohammed Salah na timu hizo kwenda mapumziko kwa sare ya 1-1.
Dakika ya 73 Mohammed Salah alipachika bao la pili lakini Tarkowski alisawazisha bao hilo akipokea pasi ya Iroegbunam dakika ya 90+8 na matokeo kuwa 2-2. Bao hilo lilizaa ugomvi baina ya wachezaji na kumlazimu refarii Michael Oliver kutoa kadi kwa Doucoure wa Everton,Jones wa Liverpool kocha Arne Slot na Kocha msaidizi Sipke Hulshoff.
Matokeo hayo yalikuwa na faida kwa Everton katika harakati zake za kujikwamua kushuka daraja wakifikisha alama 27 na kupanda mpaka nafasi ya 15.Timu hiyo imekuwa na mwelekeo chanya tangu kuwasili kwa kocha David Moyes na kuisaidia timu hiyo kufanya vyema michezo mitano iliyopita wakishinda dhidi ya Tottenham 3-2, Ushindi dhidi ya Brighton 1-0, ushindi mkubwa wa 4-0 dhidi ya Leicester City ,sare ya 2-2 dhidi ya Liverpool na kupoteza mchezo mmoja pekee dhidi ya Bournemouth 1-0.
Matokeo yafufua matumaini ya Arsenal na Nottingham
Sare ya mabao 2-2 imewafanya Liverpool kufikisha alama 57 katika michezo 24 waliyocheza ikiwa ni alama 7 pekee baina yao Arsenal na alama 10 dhidi ya Nottingham Forest timu zote zikiwa na michezo 24. Mwezi mei 10 Liverpool watawakaribisha Arsenal dimba la Anfield na mchezo huo utaamua nani anastahili kuwa bingwa wa ligi kuu Uingereza.
Mpaka sasa timu hizo zimebakiwa na michezo 14 kila mmoja na matokeo chanya baina yao yataleta ushindani wa kipekee kuelekea kumpata bingwa mpya wa ligi kuu Uingereza.
Mohammed Salah apewe kiatu chake ama tusubiri ?
Mohammed Salah ameendelea kuwa mwiba mkali kwa wapinzani wa Liverpool akifikisha mabao 22 kwenye mechi 24 alizocheza. nyota huyo anakimbizwa na Halaand mwenye mabao 19 pamoja na Alexander Isak mwenye mabao 17 sawa na Chris wood wa Nottingham. Ubora wa salah umekuwa ukionekana kwenye kila mchezo anaopata nafasi ya kuanza.