Serikali ya Tanzania, ikiongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, pamoja na viongozi wengine wa serikali, imefanya kikao muhimu na ujumbe kutoka Falme za Saudi Arabia, Lengo likiwa ni kujadili fursa za uwekezaji na kukuza ushirikiano kati ya nchi hizi mbili.

Ujumbe huu wa wafanyabiashara toka chemba ya uwekezaji kutoka nchini Saudi Arabia unaongozwa na Naibu Waziri wa Uchumi na Mipango wa Falme za Saudi Arabia, Albara Alaskandarani, na Ujumbe huu umejumuisha wafanyabiashara 30 kutoka sekta mbalimbali, ikiwemo Nishati, Kilimo, Mifugo, Uvuvi, Viwanda, Biashara na Uchukuzi.

Katika kikao hicho, Albara Alaskandarani alitoa pongezi kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa juhudi za kukuza uchumi, na kuongeza kuwa hatua hii inatarajiwa kutoa suluhisho la kudumu kwa changamoto mbalimbali za kimaendeleo.

Kwa upande wa Sekta ya Nishati uliwakilishwa na Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga kwa niaba ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt Doto Biteko.

Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Waziri wa Viwanda na Biashata, Selemani Jaffo, Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, David Kihenzile, Viongozi na wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na wawakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na wawakilishi kutoka kituo cha uwekezaji nchini TIC.

Serikali ya Tanzania inaendelea kufanya juhudi za kuvutia uwekezaji kutoka nchi mbalimbali, jambo ambalo litachochea maendeleo ya kiuchumi na ustawi wa jam

Matumaini ya Arsenal kutwaa ubingwa yarejea Salah bado hashikiki
Maisha: Jinsi ndondo cup ilivyonipatia mke