Maandalizi ya AFCON 2027 yanaendelea vyema kwa maboresho na ujenzi wa viwanja vipya, Ujenzi wa Uwanja mpya wa Samia Suluhu unaendelea vyema jijini Arusha kwa asilimia 27 na maboresho ya Uwanja wa Benjamin Mkapa yanaendelea vyema jijini Dar es Salaam.
Leo Februari 13 Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Prof. Palamaganda Kabudi ameongoza shughuli ya utiaji saini wa ujenzi wa Uwanja wa kisasa wa Dodoma wenye uwezo wa kubeba watazamaji 32,000.
Gharama za ujenzi huo ni shilingi bilioni 310 na fedha zote zitatolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo ujenzi wake utachukua miezi 24 kukamilika.
o