Saulo Steven – Manyara.
Wizara ya Afya kupitia mpango wa Taifa wa chanjo imesema kuwa kwa kipindi cha mwaka uliopita 2024 hali ya utoaji huduma ya chanjo kwa jamii, imefanikiwa kwa zaidi ya asilimia 95 katika maeneo yote nchini ikiwa ni lengo walilojiwekea.
Hayo yameelezwa na Afisa program wa Mafunzo, Uhamasishaji na Uelimishaji Jamii, Lotalis Gadau kutoka wizara ya Afya mpango wa Taifa wa chanjo, wakati akizunguza na Dar24 Media kwenye mafunzo ya siku nne kwa watoa huduma za afya juu ya uboreshaji wa Mawasiliano kati ya mtoa huduma na mteja yani Interpersonal Communication IPC mkoani Manyara.
Amesema, kiwango hicho cha utoaji wa chanjo kwa zaidi ya asilmia 95 ni maelengo yaliwekwa kutoa huduma ya chanjo walau kwa kufikia kiwango hicho huku akimshukuru Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzani Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa pesa ya chanjo mapema kwenye kota ya kwanza hivyo kufanya huduma hiyo kufanyika kwa ufanisi.
Kwa upande wake Simon Nzilibili kutoka Wizara ya Afya Idara ya Kinga sehemu ya elimu ya Afya kwa umma, amesema lengo la kutoa huduma ya chanjo ni kuikinga jamii dhidi ya Magonjwa ya mlipuko yanayoweza kuzuilika kwa chanjo kama vile Sulua, Polio, Kifua kikuu na magonjwa mengine.